1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Waliokimbia warejea.

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBds

Kiasi cha Wapalestina 100 ambao walikwama nchini Misr wamerejea nyumbani katika eneo la ukanda wa Gaza.

Kiasi cha Wapalestina 6,000 walikwama katika miji kaskazini ya Sinai tangu pale wapiganaji wa chama cha Hamas walipodhibiti eneo la Gaza katikati ya mwezi Juni na maeneo ya vivuko mpakani yalifungwa. Waziri wa mambo ya ndani wa Israel Sheetrit ameutetea uamuzi kikao cha baraza la mawaziri wa kuwarejesha watu hao makwao.

Nafikiri ilikuwa ni hatua sahihi kwa sababu watu waliokimbia kutoka Gaza wengi wao walikuwa wanahusika na chama cha Fatah, kwa hiyo walikuwa wakinusurisha maisha yao. Kwa hivi sasa hali ni tulivu katika ukanda wa Gaza , na kwa maoni yangu ni sahihi kuwapa watu hawa uwezo wa kurejea Gaza nyumbani kwao, na natumai kuwa kwa njia hii kutakuwa na hali ya utulivu katika ukanda wa Gaza.

Wapalestina hao walipelekwa kwa basi hadi Israel , ambapo baadaye waliingia katika ukanda wa Gaza kwa kupitia katika eneo la kaskazini katika kivuko cha Erez. Wapalestina wengine wanatarajiwa kusafiri kupitia njia hiyo katika siku za hivi karibuni.