1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wapalestina 4 wauawa na vikosi vya Israeli

21 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBO6

Wanajeshi wa Israeli wamewaua Wapalestina wanne katika uvamizi uliofanywa kwenye Ukanda wa Gaza.Kwa mujibu wa msemaji wa Israeli,uvamizi huo ulifanywa baada ya mashambulizi ya makombora ya wanamgambo dhidi ya Israel.Inasemekana,miongoni waliouawa ni kamanda wa kundi la Hamas katika eneo la Gaza.Hapo awali,Israeli iliutangaza Ukanda wa Gaza kama ni eneo la adui na itapunguza ugavi wa mafuta na nishati.