1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wapalestina wawili wauwawa

14 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZO

Wanajeshi wa Israel wamewaua wapalestina wawili wakati wa operesheni waliyoifanya leo kusini mashariki mwa Ukanda wa Gaza.

Msemaji wa jeshi la Israel amesema uvamizi huo ulilenga kutafuta mtandao wa mahandaki unaotumiwa na wanamgambo wa kipalestina ili kuzuia maroketi kuvumishwa dhidi ya Israel.

Duru za hospitali zinasema mama mmoja pamoja na mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 25 wameuwawa na kombora la Israel wakati walipokuwa ndani ya nyumba yao. Walioshuhudia wanasema watu wengine wasiopungua 11 wamejuruhiwa katika uvamizi huo.

Na habari za hivi punde zinasema daraja inayouunganisha mji mkuu Baghdad na eneo la kaskazini mwa Irak, imelipuliwa kwa bomu.