1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Wapiganaji washambulia Israel.

30 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCf9

Wapiganaji wa Kipalestina katika ukanda wa Gaza wamefyatua makombora nane dhidi ya Israel wakivunja makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu kwa muda wa mwezi mmoja. Makombora matatu yalianguka katika taifa hilo la Kiyahudi bila kuleta madhara. Mashambulizi hayo yamekuja baada ya waziri mkuu wa Israel kuamuru kuanza tena kwa mauaji ya kulenga katika ukanda wa gaza dhidi ya wapiganaji wanaorusha makombora.

Licha ya uamuzi huo , Israel haijajibu mashambulizi hayo. Chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano, Israel iliondoa majeshi yake kutoka Gaza ili kuweza kupata makubaliano hayo lakini maroketi zaidi ya 60 yamekwisha fyatuliwa kuelekea taifa hilo la Kiyahudi tangu wakati huo.