1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Wapiganaji wawili wa Kipalestina wauwawa.

5 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5y

Shambulio la anga la Israel dhidi ya gari moja kusini mwa ukanda wa Gaza limeuwa wapiganaji wawili wa kundi la Islamic Jihad.

Maafisa wa Palestina wamesema kuwa shambulio hilo lilifanyika katika njia kati ya miji ya Khan Younis na Rafah.

Jeshi la Israel limesema kuwa watu hao wawili walikuwa wanapanga shambulizi la kigaidi.