1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Watu watano wafa kwa mafuruko huko Gaza

28 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCF0

Kiasi cha watu watano wamekufa katika kijiji kimoja huko Ukanda wa Gaza baada ya mafuriko yaliyosababishwa na kupasuka kwa bwawa la maji.

Watu wengine 25 wamejeruhiwa kutokana na mafuriko hayo, kwenye kijiji cha Umm al Naser.

Juhudi za uokoaji zimekuwa zikiendelea, ambapo jeshi la Israel imesema kuwa litasaidia katika uokozi.Hata hivyo haijafahamika kama maafisa wa Palestina wamekubali.