1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wito kumuachilia huru ripota Alan Johnston

16 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrG

Tawi la kijeshi la chama cha Wapalestina cha Hamas,limetoa wito wa kumuachilia huru mara moja, mwandishi wa habari Alan Johnston.Mwandishi huyo alie raia wa Uingereza alitekwa nyara kwenye Ukanda wa Gaza miezi mitatu iliyopita.Tawi la Ezzedine al-Qassam limesema linachukua hatua za dhati kuhakikisha kuwa mwandishi huyo wa habari ataachiliwa huru.Alan Johnston ambae ni ripota wa BBC alitekwa nyara na kundi linalosemekena kuwa lina mahusiano na chama cha Hamas.