1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Fatah na Hamas kuweka chini silaha

20 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChr

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema maafikiano mengine ya amani kati ya makundi ya Fatah na Hamas yataanza kutekelezwa hivi punde.

Tayari makundi hayo hasimu yameanza kuwaondoa wanajeshi wake katika baadhi ya maeneo ya Gaza na kuwaachilia mateka.

Makubaliano hayo ya amani yamekuja baada ya siku moja ya mashambuliano ya risasi na utekaji nyara ambapo watu sita waliuwawa hapo jana.

Makubaliano ya awali ya kusitisha mapigano kati ya makundi hayo yalivunjika katika kipindi cha saa 24 na haijakuwa wazi endapo makubaliano mapya ya amani yatafanikiwa.Viongozi wote wawili Mahmoud Abbas na Ismail Haniyeh wametoa mwito kwa makundi yao kuacha mapigano kwa ajili ya mshikamano wa wapalestina.