1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Fatah na Hamas wakubaliano kuweka amani

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2L

Makundi yanayohasimiana katika mamlaka ya wapalestina huko Gaza yamefikia makubaliano mapya ya kuacha mapigano baada ya siku moja ya ghasia zilizosababisha kuuwawa kwa kiasi cha watu watano.

Makubaliano hayo ya amani kati ya Hamas na Fatah yamesimamiwa na wapatanishi kutoka Misri ambapo pande zote mbili zimetakiwa kuondoa wapiganaji wake majiani.

Mapigano ya jana jumapili ndio mabaya kabisa kutokea tangu makundi hayo yakubaliane mwezi Februari kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Mapigano yalianza baada ya kiongozi wa jeshi la al Aqsa lenye uhusiano na chama cha Fatah kuvamiwa na kuuwawa kwa kupigwa risasi.

Watu 18 walijeruhiwa kwenye mapigano hayo na wengine kadhaa wanadhaniwa wametekwa nyara.