1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Hamas na Fatah wasimamisha mapigano?

5 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUt

Makubaliano ya kusimamisha mapigano baina ya wafuasi wa Hamas na Fatah yameonesha dalili ya kutekelezwa baada ya watu zaidi 20 kuuawa kufuatia mapambano baina ya pande mbili hizo yaliyozuka mapema alhamisi iliyopita.

Habari zinasema wapiganaji wa pande zote mbili wameanza kuondoka katika mitaa ya Ukanda wa Gaza na maduka mengi yamefunguliwa tena.

Akizungumza mjini Damascus,kiongozi wa Hamas bwana KHALED MESHAAL ametoa mwito kwa wafuasi wa vyama hivyo kuacha mapigano kwa manufaa ya wapalestina wote. Bwana MESHAAL anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa mamlaka ya Palestina bwana Mahmoud Abbas nchini Saudi Arabia hapo kesho.