1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA.Hamas yasema Ng'o haitaitambua Israel

15 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsV

Chama cha Hamas kinacho tawala mamlaka ya Palestina kimesema kwamba hakitaitambua Israel wala suluhisho la pande mbili juu ya mzozo wa mashariki ya kati hata baada ya serikali ya umoja wa kitaifa kuundwa katika eneo hilo.

Hatua hiyo inadhaniwa kuwa itatatiza juhudi mpya za kuunda serikali ya mseto yenye msimamo wa kadiri itakayo fungua njia ya kupatikana kwa misaada inayo hitajika zaidi.

Marekani na washirika wake waliiwekea vikwazo serikali ya Hamas ili kuihinikiza itambuwe kuwepo kwa taifa la Israel na kulaani vitendo vya vurugu.

Habari zaidi zinafahamisha kuwa wadhamini wa mpango wa kutafuta amani ya mashariki ya kati wanatarajiwa kukutana leo mjini Kairo, Misri kujadili mkakati wa kufufa mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina.