1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Hatimaye Allan Jonston aachiliwa huru

4 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBls

Mwandishi habari wa BBC Alan Johnston amechiliwa huru baada ya kutekwa nyara katika ukanda wa Gaza kwa kiasi cha miezi minne.

Mwandishi huyo wa BBC yuko katika hali nzuri ya kiafya na ametoa taarifa akisema anajihisi vizuri kabisa baada ya kuachiliwa na kwamba amekuwa katika hofu kwa kipindi cha miezi minne alipokuwa mateka.

Amelipongeza kundi la Hamas kwa kutia juhudi na hatimaye kusababisha kuachiliwa kwake.

Aliyekuwa waziri wa habari katika serikali ya umoja wa kitaifa iliyokuwa ikiongozwa na Hamas Moustafa Barghouti akizungumzia kuhusu kuachiliwa kwa Jonston alisema anafuraha kwamba hamas wamejitahidi kuhakikisha kuachiliwa kwa mwandishi huyo lakini ulimwengu unapasa kufahamu umuhimu wa wapalestina kutaka uhuru wao.

Waziri mkuu aliondolewa madarakani wa mamlaka ya wapalestina Ismail Haniya wa chama cha Hamas amesema anayomatumaini kwamba hivi karibuni mwafaka utafikiwa juu ya kuachiliwa kwa mwanajeshi wa Israel Gilad Shalit aliyetekwa nyara kiasi mwaka mmoja uliopita na wanamgambo wakipalestina huko Gaza.