1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Israel yaendelea na mashambulizi

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBz0

Israel imendelea na mashambulizi yake ya anga katika ukanda baada ya chama cha Hamas na vikundi vingine vya wanamgambo wa kipalestina kudharau wito wa Rais wa Palestina Mahmoud Abbas kuwataka kuacha kurusha makombora Israel.

Msemaji wa wanamgambo hao aliitaka Israel kwanza iache mashambulizi yake, huko ukingo wa Magharibi na katika Ukanda wa Gaza.

Moja ya mashambulizi hayo Israel lililenga gari lililokuwa limewabeba wapiganaji wa Hamas, ambao hata hivyo walinusurika.

Pia mashambulizi hayo yalielekezwa katika nyumba mbili zinazomikiliwa na mwanachama wa kundi la Hamas.

Kati ya nyumba hizo, moja ni duka la kubadilishia fedha, ambalo msemaji wa jeshi la Israel amesema kuwa limekuwa likitumika kuingiza mamillioni ya dola kutoka Iran,Syria na Lebanon kila mwezi kwa ajili ya kundi la Hamas

Hapo jana Rais Mahamoud Abbas alikutana na waziri mkuu kutoka kundi la Hamas Ismail Haniya walikutana kuzungumzia hatua za kusitisha mapigano kati ya vikundi vyao.

Pamoja na kuendelea kwa mapigano ya hivi sasa kati ya Hamas na Israel, lakini hali ya uhasama kati ya kundi la Fatah na Hamas ni mkubwa.

Mapema mkutano wa viongozi hao ulifutwa, baada ya Israel kutoa tamko kuwa Waziri Mkuu Haniya huenda akalengwa na mashambulizi yao.

Na habari za hivi punde zinasema kuwa Israel imemkamata waziri wa elimu wa Palestina