1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Israel yavamia Gaza wapalestina watatu wauawa

27 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnr

Taarifa kutoka ukanda wa Gaza zinasema kuwa wapalestina watatu wameuawa na wengine sita kujeruhiwa kufuatia uvamizi wa vikosi vya Israel katika eneo hilo.

Wapalestina wawili waliuawa na wengine wanne kujeruhiwa wakati vikosi hivyo vya jeshi la Israel vilipovamia eneo la mashariki mwa Gaza.

Msemaji wa jeshi la Israel alithibitisha uvamizi huo na kwamba kulikuwa na majibizano ya risasi na wapiganaji wa kipalestina, hata hivyo alikanusha taarifa za kufanyika kwa mashambulizi ya anga.

Hatua hiyo imekuja huko kukiwa na taarifa za kuteuliwa kwa Tonny Blair kuwa mjumbe maalum wa kutafuta amani kati eneo hilo la mashariki ya kati.

Israel inamchukulia Blair kama mtu muhimu atakayeweza kutanzua mzozo huo.

Wakati huo huo Rais wa mamlaka ya wapalestina Mahmoud Abbas amepiga marufuku kwa watu kubeba silaha na milipuko bila ya kuwa na vibali.

Hatua hiyo ni katika kudhoofisha nguvu za kundi la wanamgambo wa Hamas katika ukingo wa magharibi.

Rais huyo wa mamlaka ya wapalestina ametangaza sheria kadhaa toka alipoitimua serikali ya kundi la Hamas kufuatia vurugu za ukanda wa Gaza.

Hiyo inafuatia mkutano wa Sharm el-Sheikh ambapo viongozi wa Misri, Jordan na Israel walielezea kuiunga kwao mkono serikali ya mpya ya dharura ya Mohamed Abbas.