1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Kikosi cha Hamas chatengua bomu nje ya bunge

16 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPV

Kikosi cha usalama cha kundi la Hamas kimesema kimefaulu kulitengua bomu lililokuwa limetegwa kwenye lango la kuingilia majengo ya bunge katika Ukanda wa Gaza.

Tukio hilo huenda likachochea machafuko kati ya kundi la Hamas na chama cha Fatah cha rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas. Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na njama ya kulishambulia bunge hilo.

Kundi la Hamas lilidhibiti eneo la Ukanda wa Gaza miezi mitatu iliyopita na hali ya wasiwasi imekuwa ikiendelea kuongezaka katika eneo hilo huku kundi la Fatah likifanya mikutano ya hadhara ya maombi katika majuma kadhaa yaliyopita, iliyopigwa marufuku na Hamas.