1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza.Majeshi ya Israel yamuua Mpalestina.

14 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjX

Majeshi ya Israel yamemuua mtu mmoja anayetuhumiwa kuwa mpiganaji wa Kipalestina kaskazi ya eneo la Gaza , tukio la kwanza tangu kuanza kufanyakazi makubaliano ya kusitisha mapigano wiki mbili zilizopita. Msemaji wa jeshi la Israel amesema kuwa wanajeshi katika eneo la mpakani walifyatua risasi dhidi ya mtu mmoja aliyekuwa anakaribia kituo hicho cha kijeshi akiwa na bunduki na bomu la kutupwa kwa mkono. Hapo mapema mtu mmoja ambaye hakutambulika amemuua jaji ambaye anahusiana na chama cha Hamas nje ya jengo la mahakama katika ukanda wa Gaza katika mji wa Khan Younis. Tukio hilo limekuja siku mbili baada ya kuuwawa kwa kupigwa risasi watoto wa mkuu wa usalama ambaye anamahusiano ya karibu na chama cha Fatah cha rais Mahmoud Abbas.