1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA.Mwanahabari aachiliwa huru baada ya kutekwa kwa nusu siku

25 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzY

Mwaandishi wa habari wa Uhispania aliyetekwa nyara na watu wenye silaha katika mji wa Gaza nchini Palestina ameachiliwa huru.

Emilio Morenatti mfanyakazi wa shirika la habari la Associated Press –AP- alipelekwa katika ofisi ya rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas na maafisa wa chama cha Fatah baada ya kutekwa kwa zaidi ya masaa 12.

Morenatti alidai kuwa amechoka lakini hakuteswa.

Mwanahabari huyo alitekwa nyara nje ya nyumba yake katika mji wa Gaza,hadi sasa hakuna kundi lolote lililodai kumteka nyara.

Wakati huo huo majeshi ya Israel yamesimamisha operesheni iliyochukua wiki moja katika Ukanda wa Gaza.

Taarifa ya jeshi la Israel imesema kuwa operesheni hiyo imewezesha kuharibiwa njia 15 za chini kwa chini zilizotumiwa kuingizia silaha nchini Palestina kutoka Misri.