1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Wanajeshi wa Israel waondoka beit Hanoun lakini wamewauwa wapalestina wengine 7 akiwemo mwanamke

8 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuy

Vikosi vya Israel vimeondoka kwenye mji wa Beit Hanoun kaskazini mwa Ukanda wa Gaza baada ya opresheni ya muda mrefu iliyosababisha kuuwawa kwa wapalestina 50 na mwanajeshi wa Israel.

Kwa mujibu wa maafisa wa Israel Opresheni hiyo ililengwa kukomesha mashambulio ya Roketi ya wanamgambo wakipalestina dhidi ya Israel.

Hata hivyo muda mfupi baada ya wanejshi hao wa Israel kuondoka kwenye eneo hilo la Beit Hanoun wanamgambo wa Palestina walivurumisha roketi ndani ya Israel katika mji wa Ashkelon.

Wakati huo huo vikosi vya Israel vimeripotiwa kuwauwa wapalestina 7 waliokuwa na sialaha pamoja na mwanamke mmoja katika operesheni ya iliofanywa na na wanajeshi hao katika maeneo mengine matatu huko kaskazini mwa Gaza.