1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza.Wapalestina waendelea kuuwawa katika mashambulizi ya Israel.

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2T

Jeshi la Israel limewauwa Wapalestina wanane katika mashambulizi katika ukanda wa Gaza, ikiwa ni pamoja na wanachama kadha wa chama cha Hamas, wakati hali ya machafuko ikiendelea katika eneo hilo la pwani.

Watu 22 wameuwawa katika shambulio la anga katika eneo la ukanda wa Gaza katika muda wa saa 48 zilizopita wakati Israel haionyesha kupunguza mashambulizi yake dhidi ya Palestina.