1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gazetini-Kisa cha Schreiber

4 Agosti 2009

Uharamia pwani ya somalia-kisa la nani ?

https://p.dw.com/p/J3Jg
Karlheinz SchreiberPicha: picture-alliance/ dpa

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo, yamejishughulisha kwa sehemu kubwa na mada za ndani .Hatahivyo,kisa cha uharamia katika pwani ya Somali kufuatia kuachiwa jana meli inayopakia shehena ya kijerumani,kumechambuliwa.Mada nyengine ni kule kuletwa nchinii kutoka Kanada kukabili mashtaka muuzajii silaha Karlheinz Schreiber na hongo inayodaiwa kutolewa kwa chama cha-CDU.Gazeti la Flensburger Tageblatt laandika:

"Makosa makubwa yaliosababisha visa vya uharamia ni ya jamii ya kimataifa. Uharamia wa karne za kale unapepea bendera yaketena katika PWANI YA AFRIKA Mashariki,kunatokana na kushindwa kwa UM na dola kuu kukomesha machafuko nchiini Somalia nchi iligubikwa na vita vya kienyeji.Mbaya zaidi ni kuona nia ya kumaliza fujo hilo nchni Somalia haipo.

1995 vikosi vya kuhifadhii amani vya UM viliihama Somalia.Ujerumani ilichangia wakati ule vikosi vyake.Leo Somalia nii mfano halisi wa dola lililofiolisika,dola lililoporomoka kabisa.Kwani, nchii hii iliopo katika Pembe ya Afrika, ni fujo tupu........"

Mod.Liokituchukua katika kisa cha Bw.Schreiber aliieletwa nchin Ujerumani kutoka Kanada hapo jana iili kukabili mashtaka,gazeti la ABENDZEITUNG linalochapishwa Munich, laandoka:

"Kuletwa nchiini kutoka kanada kukabili mashtaka kwa Bw.Karlheinz Schreiber kunaifufua tena sahifa ya kiza ya miaka 20 iliopita ya siasa za Ujerumani.

Je, hii ni baruti ya kuripua kamepni ya uchaguzi ujao ?

Yafaa kutiia shaka shaka hapo.Kwa watu wengi Bw.Schreiiber ambae alichangia Bibi Angela Merkel kuparamia kileleni mwa chama-tawala cha CDU, ni ukurasa uliofungwa.

Ikiwa kumekuwapo nia kujipigiia dembe kujipatia kura kwa kumrejesha nchiinii akabili mashtaka kama vile baadhi ya watu wanavyokituhumu chama cha SPD,njama hiyo haina matumaini ya ushindii.Wananchii wanashughulishwa na matatizo mengine yanayowataabisha. wakati huu ..."

Ama gazeti la SACHSISCHE ZEITUNG kutoka Dresden linaona kuwa, kujidai sasa Bw.Schreiber nii mhanga wa njama ya kisiasa, ni tabia halisi ya mtu huyu ambae ni maarufu kwa kujigamba na mwenye mdomo mpana.Gazeti laongeza:

"Kudai kuwa chama cha SPD kutokana na kisa chake kimeshashinda uchaguzi ujao,ni jambo la kuchekesha.Kurejeshwa nchini Ujerumani kukabilii mashtaka kwa Bw.Schreibers,kamwe hakutaathiri kampeni ya uchaguzi ujao.Hilo ni wsazi, hatahivyo, kesi yake itafunua kawa na kubainisha athari za matumizi maovu ya madaraka katika siasa za Ujerumani.Ili kurejesha usafi katika medani ya siasa kesi yake kwahivyo ina umuhimu mkubwa."

Gazeti la NEUE OSNABRUCKER ZEITUNG likitukamilishiia mada hii laandika kwamba, kesii ya Bw.Schreiber, haitakisaidia chama cha SPD kujitoa katika shimo la kutopendeza machoni mwa wapigakura.Kwani,kisa hiki ni cha zamanii sana.Hata chama cha SPD binafsi, hakitaki kuitumia kesi hiyo kujipigia debe katika uchaguzi ujao. Gazeti laongeza:

"Hatahivyo, kuna haja ya kuchunguza njama za Bw.Schreiiber katika biashara ya ndege za kivita,silaha na kukwepa kulipa kodi.Kile kitakachoibuka kattika kesi yake,kyamkini kikamhusu Kanzela wa zamani Helmut Kohl wala sio wa sasa bibi Angela Mekel ambae akiwa mwenyekiti wa chama cha CDU alikisafisha mno chama na enzi ya utawala wa Kohl.Ndio maana ni upuuzi mtupu kumsikia Bw.Schreiber akidai kwa mashtaka yanayomkabili Ujerumani, tayari chama cha SPD tayari kimeshinda uchaguzi ujao...kujigamba kama huko kunamfanya mwanabiashara huyu kutoka Kanada,kutotiwa maanani na kila mtu."

Mwandishi:Ramadhan Ali/Dt Presse

Mhariri:M.Abdul-Rah