1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gazetini leo

23 Julai 2008

Uhariri wa leo katika safu za magazeti ya Ujerumani umetuwama mno juu ya kutiwa nguvuni kwa Karadzic huko Serbia.

https://p.dw.com/p/EiIQ

Uchambuzi katika safu za wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo, umetuwama juu ya mada moja tu:kutiwa nguvuni ili kukabili mashtaka ya kuhilikisha waislamu wa Bosnia na wacroatia kwa Radovan Karazdic aliekua kiongozi wa waserbia huko Bosnia.

Schwäbische Zeitung laandika:

►◄

"Ulaya na Marekani zimeona kutiwa nguvuni kwa Karadzic ni ushahidi wazi kuwa Jamhuri ya Serbia inataka sasa kuhesabiwa ni mwanachama wa Jamii za kidemokrasi.Hatahivyo, sifa na makofi yanayopigwa katika miji mikuu ya nchi za magharibi kwa sehemu fulani ni unafiki mtupu.

Kwani, rais wa Serbia Tadic ametimiza kile kilichokua jukumu la kutimizwa na majeshi ya NATO.

Wakati serikaliza NATO zinapiga vita nchini Irak na Afghanistan ,zikitaka kuutia ulimwengu kitunga cha macho ,ilikua hatari sana kwao kumsaka na kumtia nguvuni mhalifu mkubwa alielindwa na wahalifu wenzake kama karadzic.

Serikali hizo zikitaka kufunika kawa madhambi yao huko Balkan zilipoachia mauaji ya umma huko Srebrenica.

Likiendelea na mada hii hii, gazeti la DER NEUE TAG- linakumbusha:

"Miaka 12 imepita tangu mahkama ya uhalifu wa vita ilipotoa hati ya kukamatwa Karadzic.Yule leo atakaeuonyoshea kidole utawala wa Belgrade,ambao ulimficha kiongozi huyo wa waserbia,huyo anabidi pia kuuliza liwapi jukumu la vikosi vya kimataifa vilivyokuwa Bosnia ?

Nalo gazeti la Nüremberger Nachrichten, lasema si kulipiza kisasi ni nia ya Mahkama ya Uhalifu, bali kusaka haki. Kuleta haki ni jukumu la Mahkama hiyo kwa jamaa za wahanga.Mbali na hayo, mashtaka haya ni pia kutoa onyo kwa serikali zote ulimwenguni kuwa iko siku ya hesabu .Hata vitani laandika gazeti:

" Sio kila silaha ni ruhusa kutumia .kuuhilikisha umma mzima na kuwatimua binadamu makwao ambako wanasiasa wa kiserbia walifanya wakati ule chini ya biramu la -safisha-safisha ya kikabila, ni uhalifu mtupu dhidi ya raia ambao lazima uadhibiwe."

"Furaha na shangwe huko Bosnia-msiba na huzuni nchini Serbia":Laandika Westfälische Nachrichten kutoka Münster.

Laongeza:

"Yule anaedhani sasa kutiwa mbaroni kwa Karadzic ndio bomu lililotegwa Balkan limezimwa,huyo anashangiria na mapema.

Vita vya kienyeji katika ile iliokua zamani shirikisho la Yugoslavia ingawa leo ni historia,majaraha yake hata kesho yatakuwa bado hayakupona.

Ingawa mhalifu mkubwa wa vita Karadzic ametiwa nguvuni,lakini aliweza kwa zaidi ya muongo mmoja kutembea huru na kwenda atakako nchini serbia.Na hii yabainisha dhahiri-shahiri kugawika kwa nchi hii ..."

Likituhetimishia mada hii, Allgemeine Zeitung kutoka Mainz lasema:

" Mwisho wa yule waliemuita "Bin Laden wa Ulaya" ndio hadithi iliokua baada ya kukamatwa Karadzic aliekuwa akisakwa kwa zaidi ya miaka 10. kujiuliza tu: ilikuaje aliweza kuzama chini asijulikane alipo kwa kipindi kama hicho kirefu,kunatoa ishara kuwa furaha huko Serbia si kwa wote.Kwani, kwa wananchi wengi wenzake ,Karadzic anasalia kuwa shujaa wao na hivyo ndivyo walivyiitikia kukamatwa kwake.