1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gazetini

19 Desemba 2006

Wahariri wamechambua dai la waziri mkuu wa Bavaria Bw.Stoiber kudurusu misingi ya bima ya afya na halkadhalika mkutano wa kilele wa teknolojia ya kisasa ya habari.

https://p.dw.com/p/CHcq

Wahariri wa magazeti ya leo ya Ujerumani wametuwama zaidi katika mada 2:

Moja ni kile kilichoitwa “Mkutano wa kwanza wa kabisa wa kilele wa kitaifa juu ya ufundi wa kupashana habari na taarifa-“IT-Gipfel”.Mada ya pili, ni kitisho alichotoa waziri-mkuu wa mkoa wa Bavaria,Edmund Stoiber kuangusha chini mfumo wa mageuzi ya bima ya siha ikiwa madai ya mkoa wake hayataridhiwa.

Gazeti la DIE WELT kutoka Berlin linasema kuna jumla ya mikutano ya kilele:mfano mkutano wa kilele wa nishati,mkutano wa kileke wa kiislamu,ule wa nafasi za kazi-job-gipfel na sasa kuna mkutano wa kilele wa teknolojia ya ufundi wa kisasa wa upashanaji habari.

Gazeti likaandika kuwa, hata kuhusu mkutano huu matokeo yake ni haba ikiwa sihivyo, umetoa ishara tu ya mkondo wa kufuatwa kwamba utafiti na ufundi kwa Ujerumani kama shina la viwanda ndio uhayi wake.Kwahivyo,laona Die welt- kuwa serikali ya Ujerumani imetunga mkakati wake binafsi wa High-Tech-ufundi wa hali ya juu wa kimamboleo-mkakati ambao hadi sasa ni raia wachache tu walioweza kuuelewa.Kwahivyo, limegundua gazeti, ilimibidi Kanzela Angela Merkel na mawaziri wake kuufahamisha barabara ueleweke-lasema Die Welt kutoka Berlin.

Ama gazeti la OSTSEE-ZEITUNG kutoka mjini Rostock laandika,wakati kweli sasa umewadia.

Lakini,lakosoa, hatua zote zinazohitajika kusukuma mbele mkakati huo na zilizopendekezwa katika kikao cha jana hakuna kipya. …….Hatahivyo si makosa kuchukua hatua zilizopendekezwa jana,lakini ,ladai gazeti-teknolojia hiyo mpya ya habari haikupokewa humu nchini mikono-miwili.Na katika fani hii, serikali ya Ujerumani,haiwezi kurekebisha mengi.Kinachotakiwa ni mifano bora kutoka viwanda binafsi vya teknolojia ya upashanaji habari- ni maoni ya OSTSEE-ZEITUNG kutoka Rostock.

Katika gazeti linalochapishwa mjini Gera-OSTTHÜRINGER ZEITUNG tunasoma:

“Hata haifai katika fahamu ya kimsingi ya uchumi kuiona serikali imeshika bendera usoni katika tangu kutunga hata kupanga mikakati ya siku zijazo za fani hii.Mifano ilioonekana katika viwanda vya kuunda ndege za Airbus na ule wa kuupanua mradi wa mawasiliano ya simu hatahivyo, imebainisha dhahiri-shahiri kuwa viwanda vinategemea serikali katika kutia jeki raslimali zao.Kwahivyo, lanasihi gazeti-watafiti,wanaviwanda na wanasiasa washirikiane.Ujerumani kama shina la uchumi na hivyo neema ya wakaazi wake inaegemea ushirikiano huo-ni maoni ya OSTTHÜRINGER ZEITUNg.

Likituhetimishia mada hii, gazeti la MITTELBAYERISCHE ZEITUNG kutoka Regensburg latoa nasaha hii:

“Ikiwa Ujerumani isioachwe nyuma katika soko la siku za mbele ,mafunzo ya teknolojia za kisasa yaanze tayari katika shule zake za msingi na imwezeshe kila mwanafunzi kuwa na kopmputa yakesawana na vile anavyopewa kitabu chake cha kusomea.Na hii inahitaji kuwapo pia walimu wa kuesomesha fani hiyo wanafunzi hao.Ukweli wa mambo lakini ni huu: katika shule za Ujerumani ambako baadhi ya nyakati darasa zima lategemea komputa 1 tu,ni mwengine kabisa.

Likitubadilishia mada,gazeti la BERLINER ZEITUNG linazungumzia kitisho alichotoa waziri-mkuu wa mkoa wa bavaria wa kuutia munda mfumo wa mageuzi ya bima ya afya ikiwa misingi mikuu ya mageuzi hayo hayatajadiliwa upya.Mikoa ya Baden-Würtemberg na Hesse imemuungamkono Bw.Stoiber.

Gazeti lakumbusha:

“Shabaha hasa ya mageuzi hayo haikuw akamwe kuwa na mfumo madhubuti wa bima ya afya……..

Hakujadhamiriwa kufanyika mageuzi hasa,bali kujitoa aibuni tu.Mfuko wa kugharimia bima hii kwahivyo, umetekelea nia hiyo ya kujitoa aibuni.Lakini si mageuzi yakufanya kazi barabara.”

Likitupa kiini kilichoibua mzozo huu mpya, gazeti la NEUE WESTFÄLISCHE kutoka Bielefeld linafunua kawa:

“vigogo vya serikali ya muungano ya Ujerumani viliafikiana kwamba bima za afya za mikoa ya shirikisho zisibebeshwe mzigo utakaopindukia Euro milioni 100 kwa mwaka.Taasisi moja huko mjini Kiel, imefichua lakini,kwamba utaratibu huo ungezigharimu bima za afya za mkoa wa Baden Würtemberg Euro bilioni 1.6,Bavaria Euro bilioni 1 na mkoa wa Hesse Euro milioni 700 laiti maafikiano yalioafikiwa hayangekuwapo. Gazeti halielewi sasa hawa mawaziri-wakuu wa mikoa hiyo 3, kinachowauma nini ?