1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Generali Perteaus apandishwa cheo na rais Bush

24 Aprili 2008

-

https://p.dw.com/p/Dnex

WASHINGTON

Rais George W Bush wa Marekani amempandisha cheo kamanda wake mkuu wa jeshi nchini Iraq Generali David Petraueus na nafasi yake kumuweka naibu wake. Hatua hiyo iliyopendekezwa na waziri wa ulinzi inalenga kuendeleza sera za rais Bush juu ya vita nchini Iraq. Hapo jana waziri wa Ulinzi Robert Gates alitangaza kwamba rais Bush atamteua Petreaus kuchukua wadhifa wa mkuu wa kikosi cha makamanda kilichokuwa kikiongozwa na William J Fallon aliyejiuzulu hivi karibuni baada ya kutofautiana na rais Bush juu ya sera zake kuelekea jamhuri ya kiislamu ya Iran. William Fallon anapinga matumizi ya nguvu dhidi ya Iran.Uteuzi wa Generali Petreaus utabidi uidhinishwe na bunge la seneta. Kikosi cha makamanda cha Marekani CentCom kinahusika na shughuli za kijeshi kwenye maeneo ya pembe ya Afrika,Asia ya kati pamoja na shughuli zote nchini Iraq na Afghanstan.