1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Angola yatuhumiwa kuhamisha wakazi

15 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1v

Hadi watu 20,000 wamepoteza makazi yao baada ya kuhamishwa na serikali ya Angola kinyume na sheria.Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa leo hii na makundi yanayotetea haki za binadamu,maelfu ya Waangola walifukuzwa Luanda kwa sababu majumba mapya yamepangwa kujengwa katika sehemu hizo. Vikosi vya usalama vya Angola,vimetuhumiwa na “Human Rights Watch” shirika lenye makao yake nchini Marekani na “SOS Habitat” la Angola,kuwa kati ya mwaka 2002 na 2006 vikosi hivyo viliteketeza kiasi ya nyumba 3000 na kwamba serikali iliwanyanganya wakazi maeneo yaliyolimwa bila ya kuwajulisha watu hao hapo kabla na wala hawakulipwa fidia.