1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Tume huru ichunguze madai ya mauaji Darfur

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0k

Shirika la Umoja wa Mataifa linalopigania haki za binadamu,limeyatuhumu majeshi ya usalama ya Sudan kuhusika na mauaji ya zaidi ya watu 100 kusini mwa Darfur,nchini Sudan.Kamishna wa Haki za Binadamu,Louise Arbor ametoa wito wa kufanywa uchunguzi huru kuhusika na madai hayo.Inasemekana kuwa katika muda wa miezi mitatu iliyopita,watu wenye silaha nzito walishambulia vijijini karibu na mji wa Nyala ulio kusini mwa Darfur.Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema,mashahidi wamewatambua washambulizi wengi kama ni walinzi wa mpakani wanaozungumza Kiarabu.Serikali ya Sudan lakini daima imepinga kuwa walinzi wake ndio wanahusika na mashambulizi ya Darfur.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,zaidi ya watu 200,000 wameuawa na wengine milioni 2 wamepoteza makazi yao,tangu kuanza kwa mapigano ya Darfur miaka minne iliyopita.