1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Ujerumani na Uingereza vina mitambo michafu ya umeme

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3Q

Shirika linalotetea mazingira duniani WWF likiwa na makao yake nchini Uswissi limesema,Ujerumani na Uingereza barani Ulaya ni miongoni mwa nchi zinazoongoza katika orodha ya mataifa yenye mitambo ya umeme inayochafua mazingira.Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotaja mitambo 30 inayotumia makaa kuzalisha umeme katika nchi za Umoja wa Ulaya,Ujerumani na Uingereza zinatoa asilimia 10 ya gesi ya kaboni dayoksaidi ya umoja huo.Vinu vya nishati vinavyochafua mazingira vibaya zaidi vipo nchini Ugiriki.