1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA : UNICEF yaadhimisha miaka 60

11 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkE

Shirika la Watoto la Mfuko wa Umoja wa Mataifa UNICEF leo hii linaadhimisha miaka 60 ya kuundwa kwake.

Katika repoti ya kila mwaka shirika hilo linatowa wito wa kulindwa kwa kiasi kikubwa kwa haki za wanawake na wasichana. UNICEF linasema kubaguliwa kwa wanawake kunawanyima fursa watoto wavulana na wasichana kufikia vipaji vyao.

Kwa mujibu wa repoti yake hiyo wasichana ndio wanaoathirika zaidi kwa kutopatiwa chakula cha kutosha,huduma mbovu za matibabu na mara nyingi hawaruhusiwi kuhudhuria shule.