1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Wairaki kwa maelfu wanaihama nchi

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD32

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi duniani,zaidi ya watu 40,000 kila mwezi wanaikimbia Irak.Vile vile zaidi ya watu milioni moja na nusu wamepoteza makazi yao nchini humo.Msemaji wa shirika hilo amesema,Wairaki kwa maelfu,wanahamia Uturuki, Lebanon,Misri,nchi za Ghuba na Ulaya.Akaongezea kuwa sasa Wairaki ni kundi kubwa kabisa kutoka taifa moja kuomba hifadhi katika nchi za Ulaya.Amesema ghasia za kimadhehebu na idadi kubwa ya mauaji,ni sababu kuu za kuikimbia Irak.