1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA:Marekani iliarifiwa mara kadhaa kuhusu madai ya kukashifiwa Koran

20 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFC0

Msemaji wa kamati ya chama cha msalaba mwekundu amesema chama hicho kiliieleza wizara ya ulinzi ya Marekani kwamba mahabusu katika jela ya Guntanamo Bay waliripoti juu ya maafisa wa Marekani wanavyoikashifu kuran tukufu.

Msemaji huyo amesema chama cha msalaba mwekundu kiliwasilisha malalamiko ya mahabusu hao mara kadhaa kati ya mwaka 2002 na mwaka 2003.

Madai ya kukashifiwa kwa kuran tukufu na maafisa wa Marekani yalichapishwa na jarida la News Week mapema mwezi huu na kuzusha maandamano na fujo katika ulimwengu wa kiislamu.

Jarida hilo liliomba msamaha kuhusu ripoti hiyo baada ya kushindwa kudhibitisha kiini cha ripoti yake hiyo.