1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA:Rwanda yafuta adhabu kali na ya kifo

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBel

Umoja wa mataifa unapongeza nchi ya Rwanda kwa kufutilia mbali adhabu kali jambo litakalorahisisha kurejeshwa nchini kwa watuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya mwaka 94 ili kuhukumiwa.Kamishna wa Kutetea haki za binadamu katika Umoja wa mataifa Louise Arbour anapongeza hatua hiyo itakayoimarisha udumishaji wa sheria.

Washukiwa wengi wa mauaji ya mwaka 94 wanaaminika kuwa barani Ulaya,Marekani ya Kaskazini na Afrika Magharibi.Bunge la Rwanda liliidhinisha kufuta adhabu ya kifo ili kurahisisha shughuli ya kuwarejesha nyumbani washukiwa hao kutoka mataifa yanayokataa kurejesha katika nchi zinazotoa adhabu ya kifo.