1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGhana

Afrika yatakiwa kuungana kuhusu fidia ya biashara ya utumwa

Bruce Amani
15 Novemba 2023

Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana ametoa wito kwa viongozi wa Afrika kuwa na msimamo wa pamoja kuhusu madai ya kulipwa fidia kutokana na biashara ya utumwa na uharibifu uliofanyika wakati wa enzi ya ukoloni.

https://p.dw.com/p/4YqK7
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS)
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo Picha: Nipah Dennis/AFP

Baadhi ya viongozi wa Magharibi katika siku za karibuni wamekiri maovu yaliyofanywa wakati wa enzi ya ukoloni Afrika na majumba ya makumbusho yameanza kurejesha mali zilizoibwa na kazi za sanaa.

Lakini dhana ya kulipa fidia ya kifedha kuhusu biashara ya mamilioni ya watumwa waliosafirishwa kutoka Afrika Magharibi na Afrika ya Kati bado halieleweki.

Ghana kuzingatia nidhamu kuhusu mkopo wa IMF

Akufo-Addo amesema katika kongamano la viongozi wa Afrika la kujadili masuala ya fidia mjini Accra kuwa hakuna kiasi cha fedha kinachoweza kurekebisha uharibifu uliosababishwa na biashara ya utumwa na madhara yaliyofuatia.

Lakini, hilo ni suala ambalo ulimwengu lazima ulikabili na hauwezi kulipuuza. Amesema hata kabla ya kukamilika mazungumzo ya fidia, bara zima la Afrika linastahili kuombwa radhi rasmi kutoka kwa mataifa ya Ulaya yaliyohusika na biashara ya utumwa.