1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghasia zaikumba Ugiriki

Halima Nyanza (ZPR)30 Juni 2011

Ghasia zimezuka jana katika mitaa ya mji mkuu wa Ugiriki Athens, baada ya wabunge kuidhinisha mpango wa miaka mitano wa euro bilioni 28 ili kubana matumizi na kuongeza kodi.

https://p.dw.com/p/11m9Y
Waziri mkuu wa Ugiriki George Papandreou (kulia) na waziri wake wa FedhaPicha: picture alliance/dpa

Polisi wa kutuliza ghasia wametumia gesi ya kutoa machozi na ya pilipili kuwatawanya waandamanaji wenye hasira. Maduka kadhaa, migahawa na majengo mengine yaliharibiwa, katika ghasia hizo.

Griechenland Demonstrationen 29.06.2011
Polisi wakitumia gesi ya kutoa machozi, kuwatawanya waandamanajiPicha: dapd

Wapinzani wa serikali waliokuwa wakitumia mabomu ya mkono na nondo walishambulia ofisi za wizara ya fedha ambazo ziko karibu na bunge la nchi hiyo, na kuvunja madirisha pamoja na kutaka kuchoma moto jengo.

Mpango huo wa kubana matumizi, ni muhimu kwa Ugiriki ili kuweza kupata Euro bilioni 12, ikiwa ni mkopo wa dharua kutoka Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa.

Hata hivyo, umekuwa ukipingwa na raia wengi wa nchi hiyo.

Wakati huohuo, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema Ugiriki inapaswa yenyewe kwanza ithibitishe kuukubali mpango huo, wa kubana matumizi na ifanye hivyo pia kwa Ulaya.