1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghasia zingine Kenya za sababisha vifo kadhaa Nakuru

26 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cy0N

NAIROBI:

Idadi kamili ya wahanga wa mapigano mapya ya kikabila katika mkoa wa Rift Valley nchini Kenya haijatambulika.Taarifa za kutatanisha zinasema kuwa watu 25 ndio wameuawa ili hali zingine kuweka idadi kuwa 35.Taarifa za awali zilisema kuwa watu wasiopungua 10 ndio wameuawa katika ghasia za mkoa wa rift Valley.Raila Odinga,kingozi wa chama cha ODM amesema kuwa ghasia zinazoendelea hazisababishwi na wafuasi wake.

Serikali ya Kenya kwa upande wake imeweka amri ya kutotembea usiku katika mkoa huo.Takriban watu wawili waliripotiwa jana kuuawa katika mji wa Nakuru ambao ndio mji mkuu wa mkoa huo.Ghasia hizi zinauhusiano na matokeo ya uchaguzi wa mwezi jana ambao yanapingwa na upande wa upinzani.Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa –Kofi Annan yuko nchini humo kujaribu kupatanisha pande mbili-wa serikali na upande wa upinzani wa chama cha ODM kuhusu kukomesha ghasia ambazo zimesababisha watu kadhaa kuuliwa.Aidha Bw Annan ametembelea mji wa Eldoret ambapo watu kadhaa walichomwa moto wakiwa ndani ya katika moja katika ghasia za kisiasa nchini humo.