1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GHAZNI:Mateka wa Korea Kusini bado hawajaachiliwa

12 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBa0

Duru ya tatu ya mazungumzo kati ya wapiganji wa Taliban na maafisa wa Korea Kusini imeanza.

Pande hizo mbili zinajadili juu ya kuachiwa huru mateka 21 raia wa Korea Kusini wanaozuiliwa na kundi hilo la Taliban.

Mateka wawili wanawake hawajaachiwa huru kama ilivyo tangazwa awali.

Mazungumzo hayo yanafanyika katika afisi za shirika la huduma za kijamii la Red Crescent katika mji wa Ghazni kilomita 140 kutoka mjini Kabul.

Kundi la Taliban limesisitiza msimamo wake kwamba mateka hao wa Korea Kusini wataachiwa huru tu pale serikali ya Afghanistan itakapo waachia wafungwa wa Taliban idadi sawa na mateka 21 raia wa Korea Kusini wanao wazuilia.

Serikali ya Afghanistan imekataa katakata agizo hilo.