1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GHAZNI:Taleban waipa serikali hadi kesho asubuhi kutimiza madai yao

31 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdR

Kundi la Taleban nchini Afghanistan wanaipa serikali nchini humo muda mpya wa mwisho hadi kesho asubuhi saa oja asubuhi saa za London ili madai yao kutimizwa kwa madhumuni ya kuwaokoa mateka 21 wa Korea Kusini waliosalia .

Hatua hii inatokea siku moja baada ya mateka wa pili kuuawa.Kundi la Taleban linaitaka serikali kuwaachia huru yapata wafungwa wao 8 wanaozuiliwa kwenye magereza nchini Afghanistan jambo ambalo serikali inapinga.

Mwili wa mateka aliouliwa hapo jana umepatikana kwenye eneo lililo kusini mwa mkoa wa Ghazni ukiwa na majeraha ya risasi.Wizara ya mambo ya nje imetambua jina la maiti hiyo ambalo ni Shim Sung-Min aliyekuwa na umri wa miaka 29.

Mwili wa kasisi aliyeongoza kundi hilo Bae Hyung-Kyu ulipatikana katika eneo hilohilo jumatano iliyopita.Kundi hilo lilikuwa katika shughuli za kutoa misaada katika eneo la kusini mwa Afghanistan lililo na usalama duni.

Kwa mujibu wa serikali juhudi za kuendelea kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia zinaendelea.

Mateka hao wa Korea Kusini ni wa kanisa la kiinjilisti na walikamatwa walipokuwa msafarani kuelekea mjini Kabul yapata wiki mbili zilizopita.