1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gianni Infantino alenga kuisafisha FIFA

Admin.WagnerD30 Novemba 2015

Giani Infantino mgombea wa kiti cha urais kutoka shirikisho la kandanda la mataifa ya Ulaya UEFA amesema atafanya kazi kuisafisha FIFA kuanzia siku ya kwanza, iwapo atachaguliwa

https://p.dw.com/p/1HErv
UEFA-Generalsekretär Gianni Infantino
Picha: picture-alliance/dpa/J. C. Bott

Infantino ameyasema hayo baada ya majadiliano ya karibu na mgombea mwenzake kutoka bara la Asia Sheikh Salman bin Ebrahim Al Khalifa.

Infantino ameliambia shirika la habari la AFP kwamba atashawishi mageuzi ya haraka mara moja atakapochaguliwa hapo Februari 26 katika kinyang'anyiro cha kumchagua mrithi wa kiti anachoacha wazi Sepp Blatter.

Nae mgombea mwingine wa kiti hicho Mwanamfalme Ali bin Hussein amesema ataweka wazi nyaraka zote za fedha katika shirikisho hilo la kandanda duniani FIFA iwapo atachaguliwa.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae /afpe / rtre
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman