1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gizo, Visiwa vya Solomon. Magonjwa yaaza kusambaa baada ya Tsunami.

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCU

Mashirika ya kutoa misaada yanasema kuwa magonjwa yanaanza kujitokeza katika maeneo yaliyokumbwa na Tsunami katika visiwa vya Solomon kusini mwa bahari ya Pacific. Mashirika ya msalaba mwekundu na Oxfam yamesema kuwa kukosekana kwa maji safi na salama ni tatizo linaloongezeka, na watoto wanaanza kuathirika kutokana na magonjwa ya kuhara. Inakadiriwa kuwa watu 5,000 wanahitaji chakula na mahali pa kuishi baada ya tetemeko lililokuwa katika kipimo cha 8.0 katika kipimo cha rischter siku ya Jumatatu na kusababisha mawimbi makubwa katika eneo la magharibi ya bahari katika visiwa vya Solomons. Mahema , na chakula vimeanza kuwasili katika eneo lililoathirika zaidi la Gizo, lakini usambazaji wa misaada katika maeneo ya ndani zaidi umecheleweshwa kwasababu ya ukosefu wa maboti pamoja na hali mbaya baharini.