1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Goergia yakataa mpango wa Ujerumani juu ya mzozo wa jimbo la Abkhazia

18 Julai 2008

Rais Saakashvili anasema hawawezi kuepuka kutumia nguvu ikibidi

https://p.dw.com/p/EeUO
Rais wa Georgia Mikhail Saakashvili, kulia na Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter SteinmeierPicha: AP

Rais wa Georgia Mikheil Saakashvili amekataa mpango unaopendekezwa na Ujerumani unaolenga kumaliza mvutano hatari kati ya Urussi na nchi hiyo ya Georgia kuhusiana na jimbo lake lililojitenga la Abkhazia.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir rais Sakaashvili amesema nchi yake haiwezi kupinga matumizi ya nguvu katika mzozo wa jimbo hilo kutokana kile alichosema ni uchokozi wa Urussi.

Ameongeza kusema ikiwa uchokozi huo utaendelea itakuwa vigumu suluhisho kupatikana.

Waziri Steinmeir ambaye anafanya ziara ya siku mbili katika eneo hilo anakwenda pia Urussi na Abkhazia kwa lengo la kutafuta suluhisho la mvutano unaondelea kati ya maeneo hayo.

Amesema hali ya mambo katika jimbo la Abkhazia inatisha na kwamba ghasia zinabidi kuzuiwa.