1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Goma, Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo. Mapigano yanaendelea.

8 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HV

Jenerali muasi Laurent Nkunda amesema leo kuwa majeshi yake yamefanya shambulio kubwa dhidi ya majeshi ya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo mashariki ya nchi hiyo.

Nkunda ambaye alipatikana katika moja kati ya ngome zake kuu, amesema jeshi la Kongo linashambulia vijiji katika jimbo la Masisi, kiasi cha kilometa 30-40 magharibi ya mji mkuu wa jimbo hilo Goma.

Afisa wa jeshi la Kongo amethibitisha kuzuka tena kwa mapigano hayo.

Zaidi ya wapiganaji 70 wa jeshi la waasi wameuwawa katika siku za hivi karibuni katika jimbo la Kivu ya kaskazini , kwa mujibu wa jeshi hilo, wakati mapigano yamesambaa mwishoni mwa juma hadi katika hifadhi ya taifa ya wanyama Sokwe ya Virunga.