1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gordon Brown kupunguza idadi ya wanajeshi wake kutoka nchini Irak

9 Oktoba 2007

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown atangaza kwamba serikali yake itawapunguza askari wake kutoka nchini Irak

https://p.dw.com/p/C77y
waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown
waziri mkuu wa Uingereza Gordon BrownPicha: AP

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema kwamba serikali yake inaazimia kupunguza idadi ya wanajeshi wake kutoka nchini Irak hadi kufikia askari 2,500.

Bwana Brown ameyasema hayo wakati alipolihutubia bunge, amesema hatua ya kwanza itaanza mara moja wakati ambapo Wairak wenyewe wameanza kutekeleza majukumu ya kulinda usalama.

Matamshi ya waziri mkuu wa Uingereza yamefuatia pendekezo lake la wiki moja iliyopita kwamba anatarajia kupunguza idadi ya askari 4,500 kufikia mwisho wa mwaka huu.

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Browm amesema kuwa maamuzi ya mwisho kuhusu kuwaondoa askari wa Uingereza kutoka nchini Irak yatapitishwa baada ya kushauriana na wakuu wa jeshi la Uingereza wa nchini Irak.