1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Grafite "mwanasoka wa mwaka wa Ujerumani"

3 Agosti 2009

Duru ya kwanza ya Kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani imepita.

https://p.dw.com/p/J2pr
Wolfsburg's Grafite akishangiria bao.Picha: AP

-Wiki kabla firimbi kulia kuanzisha msimu mpya wa Budesliga,mbrazil Grafite alieibuka msimu uliopita mtiaji mabao mengi katika bundesliga achaguliwa "mwanasoka wa mwaka wa Ujerumani".-Bayern Munich imekata tiketii yake ya duru ya pili ya kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani baada ya kuitoa jana timu ya daraja ya 6 ya Neckarelz kwa mabao 3:1

-Tajiri mkubwa wa zamani wa vyombo vya habari wa kijerumanii LEO KIRCH awekeza katika meli iliogeuzwa Hoteli kwa wageni wa kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afriika kusini.Na mwaka umetimu tangu jiji la Beijing kuandaa "michezo bora kabisa " ya olimpik katika historia.

Duru ya kwanza ya Kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani -DFB Pokale,haikuanza kwa kiishindo mwishoni mwa wiki: kwani, takriban timu zote za daraja ya kwanza pamoja na mabingwa Bayern Munich, zimeingia duru ijayo-wiki kabla msimu mpya wa Bundesliga kuanza:Duru ya kwanza ya kinyanganyiro cha Kombe la Shirikisho la dimba la Ujerumani-mojawapo ya vikombe 2 ambavyo Bayern Munich imepania kutwaa msimu huu ili kufuta madhambi ya msimu uliopita ilipopoteza vikombe vyote 2 imepita.

Bayern Munich ikiwa imejiimarisha kwa msimu mpya chini ya kocha wake mpya Van Gaal,kutoka Holland, nusra jana iaibishwe na timu ya daraja ya 6 Neckarelz jana.Mwishoe, Munich iliicharaza timu hiyo ya daraja ya 6 mabao 3-1.Kwa upande wake, Munich ilivuta pumzi pale nahodha wao mpya na wa zamani Mark van Bommel ,aliposema " hatukutiwa aibu na tumeingia duru nyengine."

Wengine lakini wana maoni tofauti.Kwani, ushindi wa mabao 3:1 dhidi ya timu ndogo kama hiyo na iliocheza kwa ujeuri,iliwatia mashakani muda mrefu majogoo wa Bayern Munich.Kwani, hadi mapumiziko ,pande hizo 2 zilisimama sare 0:0. Ni baada ya kipindi cha kwanza ndipo Mario Gomez aliejiunga msimu huu na Munich kutoka Stuttgart,kulifumania lango la chipukizi hao mara mbili-kwanza mnamo dakika ya 51 na tena dakika ya 57.

Jioni hii mpambano wa mwisho wa duru ya kwanza unakamilishwa kwa changamoto kati ya Hamburg na Dusseldorf.

Wiki kabla ya firiimbi kulia kuanzisha msimu mpya wa Bundesliga-Ligi ya Ujerumani mwishoni mwa wiki ijayo, mtiaji mabao mengii msimu uliopita kutoka klabu bingwa Wolfsburg-mbrazil Grafite amechaguliwa "mchezaji bora wa dimba wa mwaka wa Ujerumani."Kura iliofanywa na jarida la dimba mashuhuri la Ujerumani KICKER na kushirikishwa kwa waandishi wa michezo 1,042 ilimpatia Grafite kura 331 kwa 171 za mpinzanii wake Mario Gomez aliehamia msimu huu mpya Bayern munich kutoka Stuttgart.

Mchezaji mwenzake Grafite, mbosnia Edin Dzeko alierefusha mkataba wake na klabu bingwa Wolfsburg hivi punde, alitokea 3 katika kura hiyo kwa kura zake 169.Felix Magath,kocha wa mabingwa msimu uliopita na sasa Schalke msimu huu mpya amechaguliwa "Kocha wa mwaka".

Grafite alitia jumla ya mabao 28 katika mapambano 25 alioichezea Wolfsburg na hivyo si ajabu kwa Wolfsburg kumrefushia mkataba wake hadi 2012.

Baada ya kuitawaza Wolfsburg mabingwa wa Bundesliga kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo,klabu ya schalke inayotamani kuvaa taji kwa muda mrefu anaweka matumaini kwa kocha Magath nae kuwapatiia taji.

Nae Kocha Magath amesema:

"Mashabiki wanaegemeza matumaini makubwa bila ya shaka yoyote kwangu wakitumai katika timu hii halii mpya itachomoza.Kwahivyo, haisaidii kitu matumaini hayo kuyaangusha."Wiki hii unatimu mwaka tangu pale tarehe 8, mwezi wa 8 mwaka 2008 jiji la Beijing , lilipofungua rasmi michezo ya ya olimpik ya majira ya kiangazi ilioelezwa ni bora kabisa katika historia ya michezo hii.

China, imejipatia viwanja mbali mbali vya kisasa na njia za usafirii bora zikiwasafirisha mamilioni ya wakaazi wa China.Dosari moja lakini imebakia-nayo ni ule ukungu ulibakia kutandaa katika anga la Beijing..Hata kukanyagwa kwa haki za binadamu kulikokosolewa mno kumesalia.Kwahivyo, yale matumaini kabla ya michezo ile kuwa Olimpik ingesaidia kuboresha hakii za biinadamu na za jamii za wachache, hayakutimilia.

Tajiri wa kijerumani aliehodhi zamani vyombo vya habari kama TV ,Leo Kirch anasemekana amewekeza vitita vya fedha katika hotelii za melini ili kutoa huduma kwa wageni na mashabiki wa kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika Kusini-hii ni kwa muujibu wa jarida la DER SPIEGEL la Ujerumani.

Kampuni la Bw.Kirch-KF 15, limesaidia kugharimia meli 2 zitakazotia gati pwani ya Cape Town ,Durban na Port Elizabeth zikitumika kama hoteli wakati wa Kombe la dunia .Hapo kabla, Rais wa FIFA Sepp Blatter, alipendekeza meli zaweza kujaza pengo la ukosefu wa nafasi 15.000 wakati wa kombe la dunia.

Muandiishi:Ramadhan Ali

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman