1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guatemala City. Bush bado akumbana na maandamano.

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJp

Rais wa Marekani George W. Bush yuko nchini Guatemala , ikiwa ni kituo chake cha nne katika ziara yake ya mataifa matano ya Latin Amerika. Leo hii Bush alitarajiwa kujadili kuhusu uhamiaji na bishara huria na mwenzake wa Guatemala ,Oscar Berger.

Kiongozi huyo wa Marekani pia atazuru ushirika wa wakulima wa vijijini na kufanya ziara ya maeneo ya kale katika magofu ya Mayan ziara ambayo viongozi wa kabila la Mayan hawakupendezwa nayo , na wameahidi kulisafisha kiroho eneo hilo baada ya ziara hiyo kwa kuwa wanamuona Bush kuwa ni mpenda vita.

Ziara ya wiki nzima ya Bush katika eneo hilo imekumbana na maandamano makubwa.

Wakati huo huo , kiongozi mshupavu wa Venezuela mwenye kufuata mrengo wa shoto Hugo Chavez , ambaye yuko katika ziara sambamba na ya rais Bush katika eneo hilo, anaendelea na mashambulizi ya dhidi ya kiongozi huyo wa Marekani.

Akizungumza katika ziara yake katika nchi jirani ya Nicaragua, Chavez ameshambulia kile anachokiita kuingiliwa na himaya ya Amerika ya kaskazini.