1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boksiti ya Guinea

Abdu Said Mtullya18 Januari 2013

Guinea ni nchi iliyopaswa kuwa tajiri kutokana na madini ya Boksiti yanayotumika kwa kutengenezea aluminium. Licha ya akiba kubwa wananchi wake milioni 14 hawanufaiki na rasilimali hiyo.

https://p.dw.com/p/16zGY
Die Bilder wurden alle aufgenommen in der Mine von Debélén in der Provinz Kindia in Guinea-Conakry. Fotograf ist Bob Barry, freier DW-Mitarbeiter Aufnahmedatum: 06.09.12
Picha: DW/B. Barry

Rais wa Guinea Alpha Condé amesema ataanzisha sera mpya juu ya kuzidhibiti maliasili za nchi ili ziwanufaishe wananchi. Ili kuithibitisha kauli hiyo mwandishi wetu alipata fursa ya kuutembelea mgodi wa madini ya Boksiti wa Debele uliopo umbali wa karibu kilometa 150 mashariki ya mji mkuu - Conakry. Hapo aliweza kubainisha ni nani hasa anaenufaika na utajiri unaotokana na madini hayo.

Nafuu gani kwa wafanyakazi?

Madini hayo ya Boksiti yanayotumika kwa kutengenezea aluminiamu yanachimbwa kwenye mgodi huo wa Debele. Kampuni za Urusi ndizo ambazo zimekuwa zinayachukua madini ya Guinea kwa miaka zaidi ya 20 sasa. Mgodi wa Debele kwa sasa unaendeshwa na kampuni ya Kirusi inayoitwa Rusal.

Mohammed Sylla amekuwa anafanya kazi kwenye mgodi huo kwa zaidi ya miaka mitano sasa.  Anasimamia shughuli za uzalishaji. Anaziangalia mashine zote kwa sababu amesema kazi yote lazima ifanywe kwa makini kwa kuzifuata taratibu zilizopo.

Jee ananufaika kutokana na kuajiriwa kwenye mgodi huo? Amesema kuwa mshahara anaolipwa ni mdogo. Sylla amesema anakabiliwa na matatizo katika familia yake kwa sababu kipato chake ni kidogo.

Minenarbeiter mit Schaufelradbagger in Débélé, Guinea 2012 (Bob Barry/DW)
Mishahara yao pengine haitoshi kulisha jamaa: Wafanyakazi kwenye mgodi wa DébéléPicha: DW

Alisomea nchini Urusi

Lakini mfanyakazi mwengine James Camara amesema mambo yake ni mazuri. Camara ni kiongozi wa shifti. Alibahatika kufanya masomo nchini Urusi kwa kulipiwa na kampuni ya Rusal. Sasa akiwa na umri  wa miaka 32 amemaliza masomo na   anafanya kazi kama msimamizi wa wachimba migodi wa juu ya ardhi. Baba yake pia aliwahi kufanya kazi kwenye mgodi huo huo.

Schichtleiter James Camara in der Bauxitmine von Débélé, Guinea 2012 (Bob Barry/DW)
James Camara amelipiwa masomo nchini UrusiPicha: DW

Kampuni ya Rusal iliwaandikia barua wafanyakazi wote na kuwapa taarifa juu ya mashindano ya watoto. Watu walipaswa kupasi mitihani ya hesabu, Fizikia na Kemia. Baada ya mitihani vijana watano walichaguliwa ili kuenda kufanya  masomo. Camara alikuwa miongoni mwao. Sasa ni mwaka mmoja tokea Camara aanze kusimamia mchakato wote wa uzalishaji. Anasimamia jinsi shughuli za uchimbaji zinavyofanywa na jinsi madini ya Boksiti yanavyochimbwa kutoka ardhini na kusafirishwa.

Mapato madogo kwa wananchi

Kutokana na bei ya madini ya Boksiti kushuka kwenye soko la dunia, kampuni ya  Rusal inakusuduia kuurahisisha mchakato wa uchimbaji. Ndiyo sababu kampuni  hiyo imeagiza mashine za kisasa kutoka Ujerumani. Camara anajivunia magari hayo. Mashine hizo zinaweza kuchimbua hadi tani 750 kwa saa. Kutokana na matimizi ya mashine hizo za kisasa kazi ya uchimbuaji inaenda haraka kwa karibu asilimia 70. Lakini matokeo yake ni kwamba karibu wafanyakazi 300 wameshapoteza nafasi zao za ajira.

Vijana wengi hawana kazi ikiwa pamoja na Alseny Camara wakati kampuni ya Rusal inachuma faida. Swali ni je, ni kitu gani kinachobakia kwa wananchi wa Guinea wenyewe kutoka kwenye mgodi wa Boksiti?

Rundhütte und Stromleitung in Mambia, Guinea 2012 (Bob Barry/DW)
Kijiji cha Mambia kimepewa umemePicha: DW/B. Barry

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali ya Guinea na kampuni ya Rusal, kampuni hiyo inapaswa kutoa serikali asilimia 0.01 ya faida yaani kiasi cha dola moja kwa kila tani. Fedha hizo zilipaswa kuingia katika mfuko wa Wilaya. Lakini kwa muda mrefu hakuna fedha iliyoingia katika  mfuko wa Wilaya. Hata hivyo tokea  Alpha Condé aingie madarakani baada ya kuchaguliwa kwa njia za kidemokrasia, kampuni ya Rusal inatoa fedha kwa ajili ya maendeleo ya vjiji. Hivi karibuni kampuni hiyo ilitoa Euro 350,000 kwa ajili ya ugavi wa nishati ya umeme katika vijiji viwili.

2012_10_19_guinea_conakry_bauxit.psd
Infografik Afrikas Rohstoffe Guinea Bauxit Kisuaheli

Mwandishi: Bob Barry/ Abdu Mtullya

Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman