1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guinea yatimiza miaka 50 ya uhuru wake ikiwa kwenye dimbwi la umaskini.

Mohmed Dahman2 Oktoba 2008

Leo wakati Guinea inatimiza miaka hamsini baada ya kuwa huru kutoka ukoloni wa Kifaransa ikijitangazia kwamba ni bora iwe maskini kuliko kuwa tajiri na utumwani inaendelea kusota katika umaskini.

https://p.dw.com/p/FT6z
Rais wa hivi sasa wa Guinea Lansane Conte.Picha: AP Photo

Wakati Guinea kishehereka miaka hiyo 50 ya uhuru wake wahanga wa dikteta Ahmed Sekou Toure wadai kutambuliwa.

Ni afadhali kuwa na umaskini katika uhuru kuliko kuwa na utajiri utumwani kiongozi wa kizalendo wa Guinea Ahmed Sekou Toure alitamka matamshi hayo mashuhuri kumweleza Generali De Gaulle wa Ufaransa hapo mwaka 1958 wakati alipodai kupatiwa uhuru kwa haraka akikataa pendekezo la De Gaulle kuwa sehemu ya umoja wa Ufaransa na Afrika.

Nusu karne baadae nchi hiyo ya Afrika Magharibi ambayo hapo zamani ilikuwa ni nchi tajiri kabisa ya eneo la Afrika magharibi chini ya ukoloni wa Ufaransa imezongwa na matatizo ya kiuchumi na kisiasa.

Wakati hiyo ikiwa imebarikiwa na utajiri wa madini ya aluminium ghafi,chuma,dhahabu na uranium wengi wa wananchi wake milioni 9 wanaishi kwa kutegemea pungufu ya dola moja kwa siku.

Nchi hiyo iko chini katika orodha ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa ambako inashika nafasi 160 kati ya nchi 177.

Kipindupindiu kimechaga katika miji mikubwa na ni nusu tu ya idadi ya wananchi wake wanapata maji safi ya kunywa.Takriban asilimia 70 ya Waguinea hawajui kusoma na kuandika na umri mkubwa wa kutegemewa mtu kuishi ni miaka 54.

Djibril Tamsir mtaalamu wa historia na mwandishi ameliambia shirika la habari la AFP kwamba pale walipokosea ni vile walivyosimama uhuru yaani wamefanya nini miaka yote hiyo 50.

Katika kipindi cha miaka 26 madarakani Sekou Toure ambaye alikuwa akijulikana kama baba wa uhuru inafikiriwa kwamba amehusika na vifo au kutoweka kwa watu 50,000.

Generali Ulimwengu wa Tanzania ni mwanaharakati wa vuguvu la kizalendo barani Afrika na mwandishi habari mwandamizi na mchapishaji.

(O.Ton Ulimwengu )

Wahanga wa Sekou Toure wamepoteza imani kwamba waliowatesea watu wao wataweza kushtakiwa na hivi sasa wanaweza tu kuwa na matumaini kwamba watatambuwa uhalifu wao na kuomba msamaha.

Katika nyaja ya kisiasa Guinea katu haikuwahi kuwa na uchaguzi wa kidemokrasia na hivi sasa iko chini ya Generali Lansana Conte ambaye amekuwa akiitawala nchi hiyo kwa mabavu tokea mapinduzi yasio na umgwagaji damu hapo mwaka 1984.