1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hadi watu 143 wauawa Kano

Alakonya,Bruce/zpr22 Januari 2012

Duru za hospitali zinasema, takriban watu 143 wameuawa kwenye mashambulzii yaliyoratibiwa katika mji wa Kano, ulio wa pili kwa ukubwa nchini Nigeria.

https://p.dw.com/p/13nrh
Smoke rises from the police headquarters as people run for safety in Nigeria's northern city of Kano January 20, 2012. At least six people were killed in a string of bomb blasts on Friday in Nigeria's second city Kano and the authorities imposed a curfew across the city, which has been plagued by an insurgency led by the Islamist sect Boko Haram. There was no immediate claim of responsibility for the apparently coordinated attacks. REUTERS/Stringer (NIGERIA - Tags: CRIME LAW CIVIL UNREST TPX IMAGES OF THE DAY)IL UNREST)
Boko Haram wakiri kuhusika na mashambulio ya KanoPicha: Reuters

Walioshuhudiwa wamesema, maeneo kadhaa ya Kano yalifanana na eneo la vita, baada ya mashambulizi hayo yaliyofanywa na wanamgambo wa kiislamu. Kundi la kiislamu lenye msimamo mkali Boko Haram limekiri kuyapanga mashambulizi hayo ya ijumaa. Serikali imetangaza amri ya kutotoka nje saa 24.

Mashambulizi hayo, ambayo yalilenga karibu maeneo manne mjini humo, zikiwemo ofisi za polisi na uhamiaji, na uwanja wa kuegesha magari, yalifanywa ijumaa jioni. Hayo ni mashambulio mabaya kabisa kuitikisa Nigeria katika miezi ya karibuni, yakifuatia msururu wa mashambulizi dhidi ya makanisa siku kuu ya krismasi, ambapo takriban watu 40 waliuawa.