1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki ya kukusanyika majaribuni mkutano wa G20

Sekione Kitojo
5 Julai 2017

Haki ya kila mtu kuweza kukusanyika mahali  popote na wakati  wowote bila kuomba kibali  kwa polisi ama serikali  iliyohakikishwa  katika  katiba ya Ujerumani itaingia majaribuni kuanzia Ijumaa katika mkutano wa G20

https://p.dw.com/p/2fzLA
Hamburg Protest gegen G20
Picha: picture-alliance/dpa/D. Reinhardt

Sheria  hiyo itaingia  majaribuni wakati viongozi wa nchi  na  serikali watakapokusanyika  mjini  Hamburg katika  mkutano  wa  kundi  la  mataifa  yaliyoendelea  na yanayoinukia  kiuchumi  duniani G20.

"Kila  Mjerumani ana  haki , bila  ya  kujiandikisha ama ruhusa  kutoka  kokote kuweza  kukusanyika  kwa  amani bila  silaha." Hivyo  ndivyo  kinavyosema  kifungu  cha katiba  ya  Ujerumani aya  ya 8. Hiki ni  kifungu  muhimu sana   kukifahamu  kabla  ya  kuanza  kwa  mkutano  wa G20  mjini  Hamburg  siku  ya  Ijumaa . "Haki  ya mkusanyiko  wa  aina  hii  inaweza  kwa kupitia  baadhi  ya sheria  ama  kutokana  na  sababu  za  kisheria  ikawekewa ukomo." Ni  kutokana  na  kwamba  hakuna  sheria inayozuwia  kutokuwa  na  ukomo katika  sheria  ya  msingi.

Hamburg - G20-Performance "1000 Gestalten"
Maonesho ya sanaa mjini Hamburg kwa ajili ya mkutano wa G20 tarehe 05.07.2017Picha: DW/A. Drechsel

Hii itatokana  na  maafisa  wanapokaa  vikao  na  kupata taarifa  kutoka  kwa  polisi.

Vipi  uhuru  wa  kukusanyika  unaweza  kutekelezwa , je sheria ya  haki  ya  kukusanyika imepewa  umuhimu na kudhibitiwa. Sheria  hiyo  imo  katika vifungu 33. Mvutano kuhusiana  na utekelezaji  sahihi  wa  katiba  iliyopitishwa na  bunge  la  Ujerumani  mwaka  1953 na  kufanyiwa marekebisho mwaka  2008  ina husiana  na  utamaduni  wa muda  mrefu. Kwa  kawaida  machafuko  ni  kitu  cha kawaida. Watayarishaji wanapinga  sana  kuwekewa masharti  ama  ukomo, katika  wakati  wa  mkutano  kama vile  njia  za  kufanyia  maandamano na  kadhalika.

Hamburg - G20-Performance "1000 Gestalten"
Maonesho ya sanaa kwa ajili ya mkutano wa G20 mjini HamburgPicha: DW/A. Drechsel

Maandamano yatafanyika lakini kwa masharti

Hali  ya  maandamano  yenyewe  pia  ni  suala  ambalo limekuwa  na  mivutano   mjini  Hamburg  kwa  muda  wa wiki  kadhaa  sasa. Kwasababu  polisi  wamezuwia  wakati wa  mkutano  huo  wa  G20  kuanzia  tarehe 7 hadi 8 Julai , eneo  ambalo  halitaweza  kufikiwa  katika  siku  zote  hizo mbili ambalo  linaukumbwa  na  kilometa  za  mraba 38 , na watu  hawataruhusiwa  kufika  katika  eneo  hilo kwa  ajili ya  mkusanyiko  wa  aina  yoyote.

Eneo  hilo  ni  kutoka  uwanja  wa  ndege  kaskazini  mwa mji  huo hadi  katika  eneo  la  utawala  katikati  ya  mji huo.

Eneo  hilo  litakuwa  na  ulinzi  mkali , kutokana  na uwezekano  wa  waandamanaji  kujaribu kuzuwia  barabara , ambayo  inaelekea  katika  mkutano  huo  wa  G20.

Deutschland G20 Gipfel Proteste
Wanaharakati ambao wamefunga kambi wakisubiri maandamano wakati wa mkutano wa G20Picha: picture-alliance/Zumapress/J. Widener

Kwa  mtazamo  wa  polisi  inaweza  kuwa  hatari  kwa maisha ya  viongozi  wa  mataifa , wanaoshiriki  katika mkutano  huo, polisi na  watu  wengine  wanaohusika.

Pamoja  na  hayo  mkutano  huo  wa  G20  unaweza kuwa hatarini. Katika  tathimini  yao polisi  wanasema hatari iliyopo , ilionekana  pia  katika  mkutano  wa  kundi  la mataifa  yenye  utajiri  wa  viwanda  ya  G8  mjini Heiligendam  mwaka  2007 , katika  mkutano  wa  NATO miaka  miwili  baadaye mjini  Baden-Wuettemberg, maandamano  ya  kukalia  mji mwaka  2014 ama kufunguliwa  kwa  benki  kuu  ya  Ulaya  EZB mwaka  2015 mjini  Frankfurt am Main.

Deutschland G20 Gipfel Proteste
Polisi wa Ujerumani wakipambana na waandamanaji mjini Hamburg (04.07.2017)Picha: picture-alliance/dpa/C. Gateau

Mwanasheria  wa  serikali  mjini  Berlin  Christian Pestalozza anasema  inawezekana  kubinya  haki ya  uhuru wa  kukusanyika , kwasababu  ya  kuangalia  usalama  wa umma  na  utulivu.  Suali  lililopo  ni  kwamba  ni  hatua zinazochukuliwa  katika  kupunguza  uhuru  wa  kujumuika au  kukusanyika  haliwezi  kujibiwa  kwa  kusema  ndio ama  hapana alieleza mwanasheria  huyo katika mazungumzo  na  DW.

Mwandishi: Marcel Fürstenau / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Mohammed Khelef