1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki za wasenge na mashoga

8 Januari 2010

Waziri wa nje Westerwelle atadai haki hizo Mashariki ya kati ambako ni mwiko?

https://p.dw.com/p/LOca

Waziri wa nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, alipokuwa upande wa upinzani kwa chama chake cha FDP,akitetea mno haki za wasenge na mashoga nchi za nje.Haki hizo haziheshimiwi katika nchi nyingi za Mashariki ya kati anazotembelea wakati huu.

Kwa muujibu wa sheria za kimataifa, haki za mashoga,wasenge,wasagaji na wenye umbo la mchanganyiko (kike na kiume) , zinakiukwa katika nchi nyingi duniani. Vitendo vya ushoga, ni mwiko katika kiasi ya nchi 80 ulimwenguni na tabia kama hiyo, huadhibiwa kisheria.Katika nchi kama vile Iran,Yemen,Mauritania,Sudan,Saudi Arabia na Afghanistan,mchezo kama huo, hutolewa adhabu ya kifo.

Azimio maalumu kuhusu hali hii ya mambo,lilifikishwa katika Bunge la Ujerumani (Bundestag) hapo mei 6, mwaka jana chini ya kichwa: "Haki za binadamu za wasenge,mashoga,wasagaji na wenye mchanganyiko wa maumbile nchini Ujerumani na ulimwenguni kote zapaswa kulindwa."

Alielipeleka azimio hilo wakati ule si mwengine bali waziri wa sasa wa mambo ya nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, na kundi la wabunge wa chama chake cha Free Democratic party (FDP), chama cha kiliberali humu nchini.Katika azimio hilo, Bunge la Ujerumani, limetakiwa kuitaka serikali kupinga vikali kubaguliwa na kubughudhiwa kwa kundi la watu wa aina hiyo.

Miongoni mwa hatua za kuchukuliwa, serikali ya Ujerumani ilitakiwa na ninanukuklu, " Ipiganie kufutwa kwa adhabu ya kifo kwa mashoga na wasagaji ....katika nchi zinazotoa adhabu hiyo."

Mswada huo ulizimwa lakini Bungeni hapo Juni,2009 na serikali ya muungano ya vyama vya CDU/CSU na SPD dhidi ya kura za chama cha FDP,chama cha Kijani cha walinzi wa mazingira na cha mrengo wa shoto kabisa Linke.Ilizimwa zaidi kutokana na hila za kichama kuliko hoja za kimsingi. Je, waziri wa sasa wa mambo ya nje wa Ujerumani,atafuata azimio lake alilolitoa wakati ule na mada hii ataizungumza katika nchi anazozitembelea hivi sasa za Mashariki ya kati ambako tabia hiyo ni mwiko ?

Nchini Uturuki, kituo chake cha kwanza, ushoga si marufuku.Lakini, kujitembeza huko hadharani kama shoga au msagaji,ni tabu sana na hasa nje ya miji mikuu.Usjhoga hasa miongoni mwa wanaume ni kinyume kabisa na maadili tangu ya dini ya wafuasi wa chama-tawala cha kiislamu cha AKP na hata kwa wazalendo wa kituruki.

Mada hii ya ushoga ,ni nyeti zaidi katika nchi mbili nyengine atazotembelea waziri huyu wa nje wa Ujerumani Bw.Westerwelle-anadai Thomas Kolb wa Shirika la "Amnesty International" linalotetea haki za binadamu ulimwenguni,muandishi na wenzake wa kitabu "haki za kuwa na tabia tofauti na wengine".Anasema,

"Kuwa nchini Saudi Arabia, tabia ya ushoga inaadhibiwa kwa hukumu ya kifo,inatokana na sharia za kiislamu zinazotumika humo nchini.Kwa kadiri gani , adhabu hiyo inatekelezwa, ni taabu kujua kutokana na mazingira ya nchi hii yalivyo."

Watumishi wa mashirika yanayotetea haki za mwanadamu, wanaotaka kufanya uchunguzi humo nchini, hawaruhusiwi hata kutia mguu katika nchi hizo na hivyo, linabakia swali :iwapo taarifa katika magazeti ya Saudia juu ya kutekelezwa kwa adhabu za kifo kwa vitendo vya ushoga, ni za kweli au la.

Mwandishi: Gessat,Michael

Mtayarishi: Ali Ramadhan /

Uhariri: A.Lio