1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hakuna alienusurika ajali ya ndege

30 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CVGe

Ajali ya ndege nchini Uturuki,imeua abiria na watumishi wote wa ndege ya shirika la AtlasJet. Ndege hiyo aina ya McDonell Douglas MD-83 ilikuwa na watu 56 na ilianza safari yake Istanbul, ikielekea Isparta.Muda mfupi kabla ya kutua, ilipotea kwenye rada.Sababu ya ajali bado haijulikani.Juhudi za kufikia eneo la ajali zinakwenda pole pole kwa sababu ndege hiyo imeangukia sehemu za milimani,kusini-magharibi mwa Uturuki.