1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hakuna njia ya mkato kupata amani Mashariki ya Kati

Martin,Prema/zpr22 Septemba 2011

Rais wa Marekani Barack Obama amesema, hakuna njia ya mkato ya kupata amani katika Mashariki ya Kati. Obama alitamka hayo, alipokuwa akikihutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York .

https://p.dw.com/p/Rn4q
President Barack Obama addresses the United Nations General Assembly at the UN Building, Wednesday, Sept. 21, 2011. (Foto:Pablo Martinez Monsivais/AP/dapd
Rais wa Marekani, Barack Obama, New York, 21 Sep. 2011Picha: dapd

Obama amesema, anakubali kuwa Wapalestina wana haki ya kuwa na taifa lao, lakini kwanza, wanapaswa kurejea katika majadiliano ya amani pamoja na Israel na kuachana pia na matumizi ya nguvu dhidi ya jirani wao. Nchini Marekani, Obama amekuwa akishinikizwa kuiunga mkono zaidi Israel.

Marekani imesema, itatumia kura yake ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kulipinga ombi la Wapalestina la kutaka uanachama kamili katika umoja huo. Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amechukua msimamo tofauti na Marekani. Yeye amesema, ujumbe wa Wapalestina katika Umoja wa Mataifa unapaswa kupandishwa hadhi kama "taifa mwaangalizi" kwa muda wa mwaka mmoja na kipindi hicho, kitumiwe kupata suluhisho la amani pamoja na Israel.