1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hakuna tena pesa za maendeleo?

21 Novemba 2008

Viongozi wa mataifa kadhaa duniani, mkiwemo mawaziri wa fedha na vilevile wawakilishi wa wafanya biashara watakutana nchini Qatar kuhudhuria mkutano mwingine wa Umoja wa Mataifa kuhusu maenedeleo.

https://p.dw.com/p/FzEq
Mjumbe katika mkutano wa kimataifa wa biashara wa Doha QatarPicha: AP

Mkutano huo unafanyika huku kukiwa na hofu kuwa mgogoro wa kifedha unaoendelea utasababisha wadau kuondoa vitega uchumi vyao kutoka mataifa maskini, na hivyo kudumaza uwezo wa mataifa hayo maskani kufikia malengo yao ya maendeleo ya Milenia.

Mataifa mengi ambayo ni maskini hayajihusishi sana katika sekta za benki ama mikopo katika mataifa yaliyoendelea. Na hivyo kumaanisha kuwa huenda hayakuathirika moja kwa moja na mgogoro wa kifedha unaoendelea. Lakini kwa upande mwingine mataifa haya hutegemea sana mauzo yake ya nje ya mali ghafi.

Na kutokana na mgogoro wa kiuchumi unaoendelea katika mataifa yenye viwanda vingi sasa, bei ya vitu inazidi kushuka.Wataalamu wana tofautiana kuhusu nani atafaidika na yupi ataumia zaidi.

Peter Lanzert, ni mshauri mkuu katika shirika la kimaendeleo la huduma ya kanisa la Ujerumani EED.Anasema kuwa uhusiano baina ya masoko ya fedha na maendeleo hayawezi kusisitizwa,

‚Afrika itaathirika kwani kutakuwa na kuporomoka kwa bei za bidhaa, shughuli za bishara zitapungua, kwani rasli mali nyingi zilizolimbikizwa Afrika zimeondolewa, walimbikizaji wamepeleka pesa zao kwingineko kuliko salama.Matajiri katika mataifa ya kiafrika pia wanashudia sarafu zao zikishuka thamani nao wanajaribu kuziweka mahali pengine salama.Kwa hivyo wanawekeza katika sarafu ya dola ya Marekani ama yen ya Japan, kwa hivyo pesa kwa mara nyingine tena zinakwenda nchi na hiyo yote inazifanya nchi za Afrika kuwa maskani zaidi,’ amesema Lanzert.

Isitoshe ulanguzi ulikuwa umepandisha bei ya vyakula,mafuta na vitu vingine kwa kiwango cha juu sana.Lakini kutokana na mgogoro wa sasa, bei za bidhaa zimeanza kushuka tena,na hivyo kuwalazimisha wawekezaji kujiondoa.

Mgogoro huu, kwa mataifa maskani ambayo yanategemea chakula kutoka nje pamoja na bidhaa zingine,umeleta ahueni,lakini kwa mengine yanayotegemea mauzo ya nje, hili ni tisho.

Afrika,kama maeneo mengine yanayoendelea,inaweza ikashuhudia athari za mgogoro wa kifedha ikiwa bei za vitu zitaendelea kushuka hadi kutakapopatikana afueni.Lakini Yilmaz Akjüz ,ambae ni mwanauchumi wa zamani wa shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na mandeleo UNCTAD anaona kama mabara yanayopata tumbo tojo na mgogoro huu wa kifedha ni ya Asia na Amerika ya Kusini.Akjüz amesema.

' Sidhani kama Afrika ina thamani kama Amerika ya Kusini.Naamini kuwa kuporomoka kwa bei za bidhaa pamoja na mgogoro huu vitaathiri sana latin amerika kuliko Afrika. Hii ni kwa sababu Afrika haikuunganishwa vizuri katika mtandao wa masoko ya fedha ya kimataifa.Nimkweli ukuaji wa Afrika utathirika kwa kiwango fulani,lakini athari zitazikabili sana nchi zenye uchumi kama ule unaopatikana katika eneo la Amerika ya Kusini ambao unauhusiano mkubwa na mataifa ya magharibi.’

Huku uchumi wa mataifa mengi ya viwanda ukidorora,kuna dhana kuwa mpango wa kusaidia maendeleo nchi za nje unaoitwa ODA unaweza ukakabiliwa na shinikizo.Pia kuna wasiwasi kuhusu athari za mgogoro huo kwa mazungumzo ya kimataifa ya Doha Qatar kuhusu biashara .

Ikiwa hakutapatikana muafaka katika mkutano wa Doha kuna uwezekano wa kupata matatizo zaidi.Na kutokana na hali ya mambo ilivyo kwa sasa ni bayana mataifa maskani hayatakubaliana na yale tajiri kuhusu njia za kufadhili maendeleo.